Adverts

Jan 29, 2011

ZIARA YA KANUMBA MAREKANI, MWENYEWE AKISIMULIA HATUA YA MWISHO LOS ANGELES MAENEO YA UKUMBI WA STAPLES CENTER.

"
Kwa kumalizia ziara yangu ya kutembelea hollywood nimetembelea ule ukumbi maarufu wa michezo mbalimbali hasahasa basket ball kutizama mchezo wa HOCKY unaopendwa sana hapa USA,Kikubwa kilichonifanya nije hapa si kwa kupenda huu mchezo wa HOCKY ila ni umaarufu wa huu uwanja,kwa kifupi uwanja huu ndio alikuwa akifanyia mazoezi MICHAEL JACKSON kwa ajili ya show yake ya THIS IS IT,lakini pia humu ndipo mwili wake ulipoagwa mara baada ya kifo chake,Pia ukumbi huu ndio timu kubwa kama Lakers na LA KINGS hucheza mechi zake..nami nikaona ni vyema nije niione jinsi ulivyo unaitwa STAPLES CENTER. Nikiingia
Pengine unaweza shangaa kwanini napiga picha na sanamu hili la mcheza basket ball maarufu na mkongwe mwenye heshima kubwa katika mchezo huu,pengine katika maisha yangu naweza nisije onana nae na kupiga nae picha ila alininivutia kwa umahiri wake katika mchezo huo,lakini zaidi ni pale alipojigundua kuwa ni muathirika wa ugonjwa wa UKIMWI akiwa ni star mkubwa duniani aliamua kujitangaza hadharani jamii imjue kama kaathirika,ujasiri huu ndio unaonifanya nipige picha katika sanamu lake hili kama mtu yoyote yule anavyoweza kufanya,mara baada ya kujitangaza jamii ilishtuka kwa taarifa hizi lakini makampuni mengi yalijitokeza kumpa misaada na akastaafu mchezo huu akiwa kaweka rekodi hii,hadi leo bado anadunda akiwa na afya njema,aliwai pia kushiriki katika video mojawapo ya Michael Jackson,,huyu ni MAGIC JOHNSON.
Uwanjani
Monitor ya juu katikati ya kiwanja
Huu ndio uwanja wa Staples center
Mr.Jingo na mimi uwanjani
kwa juu waonekana hivi
Burudani mbalimbali
wasichana hao kazi yao ni kusafisha uwanja kwa kuondoa barafu zilizoyeyuka uwanjani maana mchezo huu unachezwa katika kiwanja chenye barafu huku wachezaji wakitumia viatu vya matairi kukimbia.
Tizama uwanja ulivyo hakika kodi za wananchi zinafanya kazi
Nikifatilia mchezo huo
Huu ndio mchezo wenyewe wa Hocky
Watu wakitazama monitor ya juu pale inaporudia goli lililofungwa....
"