Adverts

Feb 4, 2011

ALI CHOKI ABOMOA TWANGA PEPETA, ACHUKUA VICHWA SITA MUHIMU.

ALI CHOKI ABOMOA TWANGA PEPETA, ACHUKUA VICHWA SITA MUHIMU.: "
Mwanamuziki na Mkurugenzi wa bendi ya Extra Bongo Ali Choki aka Mzee wa Kijiko akiwa katika picha ya pamoja na wanamuziki wapya wa bendi hiyo aliowanyakua kutoka bendi ya African Stars Twanga Pepeta na kuwatangaza rasmi leo kwenye ukumbi wa klabu ya Adventure iliyopo Sinza Mori leo wakati alipoongea na wanahabari. Ali Choki amesema ameamua kuleta mapinduzi ya kimuziki na hiyo ndiyo kauli mbiu yake kuanzia leo, ameongeza kwamba wanamuziki hao wataungana na wenzao waliopo kambini kule Time Square Mbezi Mwisho ambapo wataendelea na kambi na kwamba zinatengenezwa nyimbo za kiwango cha hali ya juu zikiendana na shoo kabambe ambayo Mnenguaji Mahiri Hassan Mussa Nyamwela ataongoza kikosi chake katika kutengeneza dansi. Amesema katika kuimarisha nidhamu katika bendi hiyo amewaondoa baadhi ya wanamuziki wake wa zamani wanne akiwemo Greyson Semsekwa ambaye alikuwa rapa na mwimbaji wa bendi hiyo kutokana na utomvu wa Nidhamu. \Katika picha ya pamoja ni Mkurugenzi waExtra Bongo Ali Choki katikati akiwa na Hassan Mussa Nyamwela wengine waliosimama nyuma ktoka kulia ni Godfrey Kanuti (Gitaa la Sollo), Saulo John Fagason (rapa), Hosea (Mpiga gitaa la Bass) Rogat Hega (Mwimbaji na Mtunzi) na Isaack (Mnenguaji) wote kutoka bendi ya African Stars .
Ali Choki akiongea na waandishi wa habari wakati alipotangaza wanamuziki wake wapya kutoka bendi ya African Stars kulia ni Hassan Mussa Nyamwela na nyuma ni Godfrey Kanuti.
Rapa Mpya wa wa bendi ya Extra Bongo Saulo John Fagason akiongea mbele ya wanahabari wakati alipoeleza nini amewaandalia wapenzi wa bendi ya Extra Bongo.
Mkurugenzi wa bendi ya Extra Bongo Ali Choki akiwa katika picha ya pamoja na mnenguaji wake mpya Otilia kutoka bendi ya African Stars leo wakati mwanamuziki huyo alipotangaza kunyakua wanamuziki wapya kutoka bendi ya African Stars Twanga Pepeta.
"