Adverts

Feb 24, 2011

BONGO MOVIE FC WAANZA KUJIFUA LEADERS CLUB

Timu ya Bongo Movie Fc wameanza kujifua katika viwanja vya Leaders kwa ajili ya maandalizi makubwa dhidi ya Wapinzani wao Bongo Fleva Fc.
Mchezo huo ambao ni maalumu kwa ajili ya kuchangia waathirika wa Mabomu ya Gongolamboto umeanza kuvuta hisia za watu na mashabiki wengi katika jiji la Dar es salaam. Kila timu inajitamba kivyake lakini sisi tunasema ushindi ni lazima siku hiyo ya jumamosi.
Mashabiki mnaombwa kijitokeza kwa wingi ili kuchangia ndugu zetu wa Gongolamboto
Picha zaidi mcheki RAY THE GREATEST
"