Adverts

Feb 2, 2011

BRECKING NEWS: MAMBO YAZIDI KUWA MAGUMU MBOZI KWA USHIRIKINA

MWANANCHI mmoja mkazi wa kijiji cha Mnyuzi kata ya Msangano wilayani Mbozi anahofiwa kuzamishwa kwenye mto kutokana na madai ya kumfanyia ushirikina na kumuua kijana wa miaka 20 mkazi wa kijiji hicho.
Habari zilizopatikana usiku huu zinasema kabla ya tukio hilo  kundi la vijana wapato 20 waliharibu nyumba za wakazi wa wawili Kalonje Alfred na Simbeye na kuzichoma moto kwa kuwauhumu kama washirikina kijijini hapo.
Baada ya tukio hilo waliendelea kutamba kijijini na hatimaye kujichukulia maambuzi hayo jana usiku kwa kumteka mwanakijiji huyo aliyetajwa kwa jina la Samweli Simwinga ambaye aliburuzwa hadi kusikojulikana ingawa taarifa za ndani zinadai alizamishwa kwenye maji na hatimaye kuachiwa aende kwa kuzolewa na maji baada ya kuuwawa.