Adverts

Feb 3, 2011

Ni kweli mapenzi humnufaisha mwanaume tuu.

Ni kweli mapenzi humnufaisha mwanaume tuu.: "
Naamini wandugu wote mu bukheri wa afya, ningependa tusaidiane katika dhana hizi na kuona usahihi wake kwani kwa upande wangu huwa zinanipa mgagasuko kuzielewa. Ni kweli katika mapenzi mwanaume huwa anamtumia mwanamke? maana kuna hizi kauli kama, anataka kukuchezea,au anataka kukuharibu nk. Sasa ina maana mwanamke yeye huwa anachezewa na yeye hachezei, au yeye huwa aharibu? kwani kuharibu ambako hawa watu huchukulia ni kupi hasa? maana kama tunashiriki katika mapenzi pamoja bila shaka hata mimi akili zangu zitaharibika katika kuacha kufikiria maendeleo na kukufikiria wewe japo ni kwa muda mfupi. Wadau sijui nyie mnasemaje katika hili.
"