Adverts

Feb 13, 2011

BREKING NYUUUZZZZZ: AJALI MBAYA RUVU LEO

BREKING NYUUUZZZZZ: AJALI MBAYA RUVU LEO: "
Lori likiondoa gari dogo aina ya Toyota Land Cruiser iliyogongana na basi la abiria la Moro Best maeneo ya Ruvu Darajani ambapo mtu mmoja ambaye ni dereva wa Land Cruiser anasadikiwa amefariki dunia hapohapo. Mashuhudu wameiambia Globu ya Jamii eneo la tukio kwamba ajali hiyo imetokea mara tu baada ya msafara wa Mama Salma Kikwete uliokuwa unatokea Dar kupita mbele kidogo ya daraja la Ruvu ndipo ajali ikatokea, ambapo hilo basi likitokea Morogoro kwanza liliipamia Hiace kwa nyuma kabla ya kurudi barabarani na kupambana na la hilo Land Cruiser ambalo insemekana lilikuwa kama gari la nne hivi nyuma ya msafara wa Mama Kikwete ambaye hakudhurika. Juhudi za kumpata msemaji wa polisi kwa maelezo rasmi ya kina zinaendelea na tutawapasha Wakaazi wa Ruvu wakiangalia gari lililopata ajali Askari wa usalama barabarani na wananchi eneo la tukio Basi la Moro Best likiwa eneo la tukio baada ya ajali hiyo.
Picha na mdau wa Globu ya Jamii
"