Na Joseph ishengoma -MAELEZO-Dodoma
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Anne Makinda ameiagiza serikali kutoa maelezo kuhusu tatizo la kuzaga kwa noti bandia mitaani.
Mheshimiwa Spika Anne Makinda ametoa agizo hilo leo bungeni mjini dodoma baada ya mbunge wa...Spika wa Bunge Anne Makinda ameiagiza serikali kutoa maelezo kuhusu tatizo la kuzaga kwa noti bandia mitaani.Mheshimiwa Spika Anne Makinda ametoa agizo hilo leo bungeni mjini dodoma baada ya mbunge wa jimbo la mji mkongwe Mheshimiwa Mohamed Sanya kumkabidhi noti baandia ya Tsh 10.000.
Kwa mujibu wa maelezo yake bungeni ni kwamba aliipata noti hiyo kutoka kwa mfanyabiashara mdogo aliyemuomba aipeleke bungeni na kuikabidhi kwa spika na kwamba kiwango cha Elfu kumi ni kipato cha wiki nzima kwa mfanyabishara huyu kijana.
'Benki kuu ya Tanzania ilichapisha noti mpya na kuzisambaza lakini hata kabla ya siku 100 kupita wajanja wachache wa ndani au wa nje wanachapisha noti hizo na hapa dodoma zipo Mheshimiwa Spika.'
Noti hiyo ya bandia iliyokabidhiwa kwa mheshimiwa spika leo ilikua haina alama ya baba wa taifa na mbunge huyo ameiomba serikali kuchukua hatua za dharura na za haraka kuwaelewesha wananchi alama mpya za noti mpya.