Adverts

Feb 16, 2011

NECTA SERVER YAONYESHA KUZIDIWA NA MZIGO MZITO WA USAAJIRI

Online Registration



Mtandao wa baraza la mitihani TANZANIA kwa siku ya jana hadi usiku wa leo umeonekana kuzidiwa kutokana na kushindwa kukamilisha hatua za kusajiri wanafunzi.



Kwa siku nzima ya jana kuanzia mchana hali ilianza kuwa ngumu kutokana na kukatika katika kwa mtandao huo hasa inapofikia hatua ya uploading picha kuendelea kwenye hatua ya kuchagua aina ya malipo.
Intenet Cafe nyingi katika mkoa wa mbeya zimeonekna kulalamikia hali hiyo  na kwamba imesababisha msongamano kutokana na wanafunzi waliotoka mbali kutokfahamu hasa lini watakamilisha zoezi hilo, wataishi wapi na kwa gharama za nani.
"unajua kaka leo ni siku ya pili tangu nije mjini kutoka USANGU lakini huduma ndiyo hii unavyoona sasa sijui nitafanyaje " alisema mmoja wa wanaotarajia kujisajiri kwa mitihani ya marejeo.
Pamoja na jitihada za watoa huduma kuiandikia timu ya mafundi ya mtandao wa necta kwaajili  ya kufanyia marekebisho hali hiyo, dalili za kuzidiwa kwa server yao zinaonyesha wazi kuwa nje ya uwezo hivyo kuahidi kulishughulikia tatizo husika.
Kwa ujumla utaratibu huo licha ya kuonyesha maboresho katika hatua za usajiri wa mwanafunzi umeonyesha kuwababaisha zaidi wananchi ambao matumizi ya kompyuta na masuala ya mtandao ni kama "mkwe" pengine kutokana na mazingira na kujenga hofu kuwa baadhi ya e mail zilizofunguliwa ili kuwezesha taarifa za kukubaliwa kwao kupatikana humo zinaweza kufungwa bila wenyewe kupata majibu yao kwakuwa hawana fulsa za kuzitumia.
Kazi inaonekana zaidi huko mjini ambapo kutokana na msongamano baadhi ya cafe zimewaingiza mjini kwa kujaza maelezo ya watahiniwa na baadaye kuzibandika picha na  kupiga vivuli/photocopy picha zao na hatimaye kutokomea na elfu tano zao  wakati fomu hizo zikipelekwa kwa wakuu wa shule zikiwa na rangi ya Black and white kwenye picha zimekuwa zikikataliwa!!!
Licha ya baraza la mitihani kuwatuma watalaamu wake mikoani kufuatilia hali hiyo lakini wameonekana kutokuwa na msaada sana hasa katika eneo la ufundi kutokana na wao pia kupokea tatizo na kuliwasilisha makao makuu yao kutegemea ufumbuzi huko, hali ambayo pia inazidi kuongeza mlolongo wa matatizo yaliyo ndani ya mafanikio ya mpango huo wa kusajiri kupitia mtandao.
Ni matarajio ya mtandao huu kuwa baraza litafanyia kazi haya yanayojitokeza katika hatua hizi za usajiri......!!