Mkuu Mpya wa Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo Dk Robert Kisusu. Dk Kisusu anachukua nafasi iliyoachwa wazi baada ya kufariki kwa aliyekuwa Mkuu wa chuo hicho Hayati Donath Musiba aliyefariki miaka miwili iliyopita.
Mjumbe wa baraza la Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Mgana Msindai akizungumza na wanachuo wa Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Kulia aliyekaa ni Mwenyekiti wa Baraza la Chuo hicho Ramadhani Khalfani na Kushoto ni Mkuu Mpya wa Chuo hicho Dk. Robert Kisusu
Wanachuo kutoka chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo. Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo ambacho hivi sasa kina wanachuo 1389 pamoja na kutoa mafunzo kwa watumishi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kitatoa mafunzo maalum kwa viongozi wakuu wa Mamlaka za Serikali za Mitaa wakiwemo wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya. Picha na mdau Mathew S. Kwembe wa Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI
"