Adverts

Feb 7, 2011

`hali zote'...mambo kufa, kufaana!

`hali zote'...mambo kufa, kufaana!: "
Joto kali sana leo, nimewasha kiyoyozi cha gari lakini haisaidii kitu..’ huyu alikuwa bosi wangu akilalamika huku anaangalia kiyoyozi cha ofisi kuwa kinafanya kazi kweli, kipo kinafanya kazi lakini kutokana na joto lilivyo hapa Dar kilionekana kama hakipo. Nikakumbuka kuwa wenzetu huko Ulaya wanalaalmika na baridi, na sio baridi ile ya hapa kwetu , bali ni baridi ya barafu. Je hali kama hiyo ingetokea hapa kwetu ingekuwaje, maana umeme wa mgawo, labda magogo msituni yangeisha kwa kuchomwa mkaa Ni kweli hapa Dar, sasa hivi kuna joto kali, na inachangiwa zaidi na ukosefuu wa miti, utashangaa ukipita sehemu za barabarani unakuta miti imekatwa, na huoni dalili ya miti mingine iliyopandwa ili ukikatwa mmoja unachipua mwingine, je kwa hali kama hii joto litakwisha kweli, Dar inageuka kuwa jangwa, na mijumba inahumuka kama uyoga. Hatukatai hayo ni manendeleo , lakini je tutaishia kuwa na viyoyozi mpaka mabarabarani. Na heri tunaodoea viyoyozi vya ofisini, ingawaje kiafya inatuathiri, kwani unatoka kwenye kiyoyozi ofisini unaingia kwenye tanuri la moto nyumbani kwako! Niliwahi kutoa wazo kuwa ingekuwa jambo la muhimu serikali ikapitisha sheria kuwa kila kaya, kila nyumba lazima ipande miti angalau miwili kwa nyumba, kama hii ingepitishwa ungeona mabadiliko makubwa sana hapa Dar, lakini kama ujuavyo, huenda kitu kama hiki kinasubiri mfadhili, huenda mipango hii ipo, au inatakiwa iwe kama mradi Fulani…lakini joto lililopo hivi sasa lingetosha kutupa shule. Hulka ya binadamu tulivyo ni kusahau, kipindi hiki cha joto, maswala ya watu kujenga bondeni ayansahaulika, watu wanajenga, watu wanauziwa maneo ambayo ni mapitio ya maji, na kwasababu mtu hujui na una shida ya eneo la kujenga unanunua , mvua zikianza ndio tunaanza kushituka, oooh, waliojenga mabondeni muondoke, ooh…kwasababu hatutaki kujifunza kutokana na mabdiliko ya hali ya hewa. Kipindi cha joto kitupe fundisho la kukabiliana na joto, kwa kuhakikisha kuwa mvua zikianza tunapanda miti kwa wingi, ili hata joto likiana tuna vivuli vya kujifichia. ‘Duuh, umeme umakatika, balaa gani hili…’bosi akainuka haraka toka kwenye kiti chake na kukimbilia nje akiwa na leso ya kufutia jasho, na bahati nzuri kuna miti imependwa hapoo karibu na ofisini, akawa anapata upepo wa asili, huku anajipepea na mkono wake, akisubiri jenerata liwashwe. Sisi watu wa hali zote tukawa tunamshangaa anavyopata taabu, hakuzoea hali kama hiyo masikini wa mungu! Mimi nikawaza kichwani, huyu kazoea kiyoyozi, toka nyumbani, garini hadi ofisini, lakini hebu rudi nyumba kwetu ambapo maisha yetu ni `hali zote’, kuna watoto wadogo ambao ukiwaangalia sasa hivi utawaonea Huruma, mwili umejaa vipele vya joto…hawa wataishije, au ndio wakomae ili wawe `hali zote’ kama wazazi wao? Labda ndio maana umeme unakatika kama mataa ya barabarani, ili tuzoee hali zote, na aheri ingekuwa kama mataa ya barabarani ungeshukuru, kwani hayo yanawaka kwa muda maalumu, lakini umeme wetu unakatika mchana kutwa! Jamaa yangu anasema kuna siku kapata hasara ya nyama, alinunua kwa ajili ya shughuli yake, akaweka kwenye jokofu, umeme ukawa haupo siku nzima, alipoichukua kesho yake, haitamaniki…ikawa hasara! Je tunajifunza nini na tatizo la umeme kipindi hiki cha shida, ili tujiandae kwa baaadaye, je ina maana hatuna utaalamu(wataalamu) wa kugundua njia mbadala, badala ya kutegemea `mvua’. Kwani hayo maji hayawezi kuvutwa na bomba toka sehemu nyingine, ili kujaza kina cha hilo `bwawa’ nimewaza sana kuhusu hili, lakini nikajisema huenda kwa vile mimi sio mtaalamu wa mambo hayo, basi najifikiria nianavyo tu…lakini mimi nina imana kuwa wataalamu wapo na wakiwezeshwa wataweza kupambana na hili tatizo, …lakini watawezeshwaje, wakati bajeti haitioshi…haitoshi kwa vitu kama hivyo, inatosha kwa magari ya wakubwa…Au? Nawaza tu mtoto wa `hali zote’ Kusahau ni hulka yetu wanadamu, maana kama tusingelikuwa tukisahau huenda hata akina mama wasingependa kujifungua tena. Lakini kuna mambo ambayo sio ya kusahau, kwa mfano sasa hivi mwavuli unaonekana ni takataka, nimekuta mwavuli mzuri tu upo jalalani, nikauliza hivi huu mbona bado unafaa kutumika…jibu ni kuwa wanini na joto lote hili. Tumesahau kuwa pindi siku zijazo, mvua zitaanza kunyesha, je tumejiandaaje na kukabiliana na mvua, au ki mawazo yetu ni kuwa, tusubiri siku ikifika itakutana na mambo yake, kwani hawo watengeneza mwavuli watapata wapi pesa, …maana mmmh,.. kufa ni, kufaana, … Ni wazo tu la ijumaa, Ni mimi: emu-three
http://miram3.blogspot.com/feeds/posts/default?alt=rss

"