Adverts

Feb 27, 2011

HARAMBEE YA GONGO LA MBOTO READING YAFANA

Frank Kutoka Urban Pulse akiwa na tina kutoka Miss Jestina Blog wakila pozi baada ya harambee. Salam, Tunapenda kutoa shukrani zetu za Dhati kwa watanzania wote waishio Reading UK walioweza Kuja Vincent kuchangia wahanga wa Gongo la Mboto Tanzania. Kwa muda wa saa moja tumekusanya Jumla ya pesa taslim Pounds £200 Pia tumekusanya Nguo nyingi kutoka kwa watu mbalimbali. Tafadhali Kumbuka bado hujachelewa kwa wakazi wa Reading ambao hawakuweza kufika leo mnaweza kupeleka michango yenu Vincent siku ya mwisho ya kukusanya ni jumanne ijayo tarehe 1.3.11. Ningependa kutoa shukrani za dhati kutoka URBAN PULSE,MISS JESTINA BLOG,AIL TV, LOCUS IMPEX SHIPPING CO, SHILLA FRISCH, MRS NASIBU NA Utawala wa Vincent Restaurant Reading kwa kusaidia zoezi la leo. Mungu Ibariki Africa, Mungu Ibariki Tanzania Asanteni Mkurugenzi Mtendaji wa LOCUS IMPEX SHIPPING MR B CHISUMO akifungua Harambee. Mdau akichangia mada. Wadau wakiendelea kutoa michango yao katika harambee hiyoo. Mtoto Chanele akimpa Mchango wake Miss Jestina. wadau wa UK wakifuatilia mpango mzima wa Harambee. Baada ya kazi, kutoka kushoto JJ, Chisumo, miss Jestina,Gardol na Frank.
"