Feb 19, 2011
HII HATUA YA MWANANGU NIMEIPENDA SANA
Hatua hii katika makuzi huambatana na uwezo wa mtoto angalau kutamka maneno 2 hadi 4 kwa ufasaha, ni hatua ambayo mtoto anakuwa mbishi kila unachofanya anataja naye afanye, watoto wengine usiku wanaamka na kutaka kufanya kile alichokuwa akifanya mchana ikiwa kitu hicho kipokaribu! Sasa huyu kamanda ananipa burudani manake leo usiku kaamka saa nane kutafuta nimeficha wapi laptop achezee kwa kubonyeza bonyeza keyboard hata kama hajui, alipokosa akaibamiza simu yangu iliyokuwa karibu imesambaratika!!!! halafu akaniangalia usoni alivyoona kama nimekasirika naye akajiaungusha chini na kuact akilia ili nimhurumie nimbebe. very interesting