Tanzania kwa sasa ina zaidi ya vituo vya redio 120 za Fm lakini matumizi yake kadiri siku zinvyoenda yanaonekana kupoteza maana ya ille dhana hii ilivyokusudiwa.
kwa sehemu kubwa vyombo hivi vimesaidia kurelay album na single za wanamziki wa bongo flava, yes na kuafanya hata walioko vijijini kufahamu hii single ya marlow, ooh hii ya Mr II lakini je vimefanya nini kwenye shughuli inayoajiri watanzania zaidi ya 80% nazungumzia kilimo?
Bado kilimo vijijini ni kile kile, hiyo minjingu inayotoka Arusha ni wakulima wangapi wanajua kwa kipindi gani inapoweka ardhini huchukua katika kuleta mabadiliko ya udongo?
Ni tafiti ngapi zimefanywa na vituo hivi kuhusiana na masuala mbalimbali ya kijamii ambayo yana mchango katika kubadili fikra za Watz? sasa hivi hapo ulipo kamata kijana wa kidato cha sita muulize idara ya uhamiaji ipo chini ya wizara gani uone anavyochemka!!!!1 lakini usimkatishe tamaa muulize ni single gani inayohit sasa hivi kwenye Tv za bongo?
Mwache huyo chukua kijana wa University iwe hizi za kata ama zile za mwalimu, ehee Nanjilinji ni moja ya maeneo yaliyo kusini mwa Tanzania, ni mkoa gani huo? badala ya kukutajia hata mkoa wowote wa Kusini utasikia Arusha!!!!!!!!!!
mie nasikitika hii yote ni kwasababu media ina influence, inaweza kuset ajenda na kuwadrag watu kusikojulikana ikiwa hakuna mwelekeo wa kuzisimamia na kuwa na mwongozo wa wakati upi tuwe na program zipi? vile vipindi vya wizara ya elimu mpaka sasa vinasikika TBC tu je hizi Fm hazina nafasi ya kufanya kazi hiyo kutokana na ukaribu wake na wananchi?
aaaah naelekea kukata tamaa toka asubuhi ni mziki weeeeee mpka jioni, nafikiri kunajambo bado la kufanya katika kuviimarisha vituo hivi na kuwa na mwelekeo wa kufundisha badala ya kuburudisha zaidi kuliko kuelimisha!! yaani iwe kubuudisha 25% kuelimisha 50% kukosoa 20% na kuhamasisha 5% . Kuhamasisha inachukua chache kwakuwa tayari katika kuelemisha pia kuna kuhamasisha ndani yake!