Na Danny Tweve Tunduma
Wanzania 7 wanaofanya biashara ya kubadili fedha mitaani katika eneo la Tunduma wamekamatwa na kushikiliwa kwa wiki ya pili sasa na polisi wa upande wa Zambia kwa tuhuma za kufanya biashara ya fedha upande wa Zambia kinyume cha sheria.
Taarifa zilizothibitishwa na Vyombo vya kiintelijensia zinazema kumakatwa kwa watanzania hao ni matokeo ya hatua za serikali ya Zambia kudhibiti tabia inayodaiwa kujengeka miongoni mwa wabongo kujihusisha na biashara ambazo upande mwingine hufanywa kulingana na taratibu za nchi husika.
\
Jitihada za mawasiliano ya kutaka waaachiwe zinaonekana kugonga mwamba ambapo sasa wanahikiliwa katika mahabusu ya Isoka iliyopo umbali wa kilometa 60 kutoka Nakonde eneo la Mpaka wa Tanzania na Zzambia.
Taarifa zaidi zinadokeza kuwa kuna zaidi ya maangalizo manne yaliyotolewa kwa nyakati tofauti na serikali ya Zambia juu ya mienendo ya watanzania inayoenda kinyume na taratibu za nchi hiyo ikiwemo ya kujaza watoto wa kitanzania kwenye shule za upande wa Zambia, kufanya biashara ya Umachinga (vendors), Kubadili fedha upande wa Zambia na vijana kujihusisha na uhalifu mwingine upande wa Nakonde.
Kutokana na hali hiyo wazambia wamekuwa wakielezea kuwa hali hiyo inaathiri kwa namna moja ama nyingine mahusiano kwakuwa inaonyesha nchi moja kudharau taratibu za nchi nyingine hali ambayo wanadai hawakubaliana nayo.
Wakati hayo yakiendelea, tayari taarifa za chini chini zinaonyesha kuwa upande wa Tanzania (Tunduma) baadhi ya vijana wanajikusanya kuanza kupanga njama za kushinikiza mpango wa kuwatoa kinguvu ikiwa ni pamoja na kuandaa maandamano yanayolenga kuzuia watu wa upande wa pili (ZAMBIA) kufanya shughuli upande wa Tz.
Habari za kiintelijensia ya uandishi zinaonyesha kuwa watuhumiwa hao saba watafikishwa mahakamani tarehe 21 mwezi February katika mahakama ya Nakonde ambapo vijana na wafanya biashara mjini Tunduma wanapanga kujikusanya ili kushinikiza kutolewa wenzao.
Aidha hali ya kushindwa kufuata taratibu za kubadili fedha eneo hilo inaonekana pia kuwa na mikono ya baadhi ya viongozi ambapo maamuzi ya pamoja yamekuwa yakiiukwa kila yanapoazimiwa kwani katika kipindi cha miaka mitatu sasa tangu agizo la kusitisha ubadilishaji wa fedha mitaani kuamuliwa, utekelezaji wake umekuwa mgumu kutokana na polisi kukamata na kuwafikisha mahakamani lakini baadaye viongozi kuingilia kati.
Inadaiwa hali hiyo imekuwa ikifanywa kwa maslahi ya kisiasa na pia miongoni mwao kuwa na maslahi binafsi katika uendeshaji wa shughuli hizo ambazo zinahusisha wafanyabiashara wakubwa ambao ndiyo forex za mpakani kwa maana ya kutoa fedha kila siku na kuwakabidhi vijana kwenda kubadilisha na baadaye kurejesha mauzo.
Jana timu ya blog ya uchunguzi ilitia timu eneo la Tunduma kufuatilia hali ya hewa ambapo imeshuhudia majadiliano ya makundi kuhusiana na vijana hao ingawa pia makundi hayo yameonekana kuketi kivyama hali ambayo inaonyesha mwelekeo wa kubadilika dhana kutoka ile ya watanzania kukamatwa na sasa kuwa ya wafuasi wa chama fulani kukamatwa. na chama kingine kikionyesha kushabikia hatua ya watanzania hao kukamatwa.
mwisho.