Mkuu wa Kitengo cah Mawasiliano Jeshi la wananchi Tazania JWTZ Luteni Kanali Masoud Mgawe Kapambala akiongea na waandishi wa habari katika lango kuu la kuingilia katika kambi ya jeshi ya Gongo la Mboto ambayo jana usiku ilikumbwa na milipuko ya mabomu.
Luteni Kanali Kapambala amesema Chanzo cha kulipuka kwa mabomu hayo kitatolewa baada ya uchunguzi kufanwa na vyombo husika na kutoa taarifa kamili, amesema hakuna askari aliyekufa isipokuwa mmoja ambaye amepata mchubuko kidogo lakini kinachoendelea sasa ni kukusanya mabomu yote ambayo yamesambaa katika maeneo tofauti jijini ili kuyaharibu kwa pamoja.
Luteni Kanali Kapambala amoengeza kwamba watu wasiwe na wasiwasi hayo mabomu hayawezi kulipkua labda mtua aanze kuyachezea kama vile kukata vyuma chakavu hiyo ndiyo itakuwa hatari zaidi lakini vinginevyo hali ni shwari.
Vyombo vya usalama vimewatanzia wananchi kutoondoka katika makazi yao na kuwataka kurejea majumbani mwao lakini inaonekana watu wengi wanaogopa kurudi majumbani mwao kwani misururu ya watu wanaoondoka kutoka huko wakelekea maeneo ya Buguruni ni wengi sana barabarani na magari yanafurika abiria huku foleni ya magari ikiwa kubwa njiani.
Msafara wa Rais Jakaya Kikwete ukirejea Ikulu mara baada ya Rais kutembelea Kambi ya Jeshi la wananchi JWTZ ya Gongo la Mboto iliyokumbwa na milipuko jana usiku na kusababisha vifo vya watu 17 na wengine kujeruhiwa huku mali na nyumba za wakazi wa maeneo ya jirani na kambi hiyo zikiteketea.
Mama Marcelina Thomas Kirenga mkazi wa Pugu Kajiungeni ambaye nyumba yake imeteketezwa kwa Kombora akihojiwa na waandishi wa habari wa TBC1 nyumbani kwake.
Jamaa huy ambaye jina lake halikupatikana mara moja akiwa ammbeba mtoto wake mgongoni akiongozana na familia yake kuondoka katika eneo hio leo mchana picha hii imepigwa hapo Ukonga Banana.
Hii ndiyo Misururu ya magari na watu wakiondoka huko Gongo la Mboto na Pugu kama unavyowaona katika picha hii.
Hawa wanaondoka huko Pugu lakini hawajui wanakoelekea wanasema ni afadhali kufia mbali kuliko huko kwenye makzi yao.
Hili limedondoka katika nyumba ya Marcelina Thomas Kirenga ambaye nyumba yake imeteketea kabisa kwa moto huko Pugu Kajiungeni.
"