Adverts

Feb 23, 2011

hongera gazeti la mwananchi kwa kututoa kimasomaso

Globu ya Jamii inalipongeza gazeti la 'Mwanan na chi' kwa weledi waliouonesha katika kupata picha ya mmiliki wa Dowans na kukata kiu cha wananchi cha kutaka kumuona mtu ambaye baada ya kukataa kupigwa picha alipokutana na wahariri aliokutana nao jijini Dar. Pamoja na kwamba Globu ya Jamii haikualikwa kwenye mkutano huo, lakini inajiunga katika foleni ya kupokea lawama kwamba kitendo cha kukosa picha ya mfanyabishara huyo hakisameheki katika tasnia ya habari yenye kuangalia weledi. Ajabu ni kwamba hata kumfuatilia kama lilivyofanya 'Mwananchi' na hatimaye kumnasa sura yake laivu, hakuna labda Globu ya Jamii ambayo nayo ilikuwepo wakati mmiliki huyo wa Dowans alipokuwa anakagua mitambo yake Ubungo hio jana kama picha zinavyojieleza hapo chini. Hongera sana mhariri na mpiga picha wa 'Mwananchi' kwani baada ya gari la maharusi kuanguka na kuua bwana na bibi harusi, hamkurudi chumba cha habari na kusema hakuna habari sababu maharusi wamekufa. -Michuzi
Shangingi jeusi lililomchukua Al Adawi likikatisha maeneo ya Ubungo kuelekea kwenye mtambo wa Dowans. Gari la mbele limebeba wapambe wake
Shangingi likiingia geti la Dowans
Walinzi wafungua geti
Al Adawi anatelemka na kuanza kukagua mitambo yake ya Dowans
"