JK akiifariji familia ya Marehemu Shekhe Kassim Mtopea aliyefariki jana nyumbani kwake Temeke, jijini Dar es Salaam baada ya kusumbuliwa na maradhi ya kisukari na shinikizo la damu. Rais Kikwete alifuatana na mkewe Mama Salma Kikwete. Marehemu Shekhe Mtopea alikuwa kada wa Chama Cha Mapinduzi CCM na tangu mwaka 2002 hadi 2007 alichaguliwa kushika nafasi mbalimbali za uongozi zikiwemo,Mjumbe wa Kamati ya Siasa kata ya Azimio,Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Temeke na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa.Marehemu ameacha mjane mmoja watoto kumi na mbili na wajukuu ishirini na moja.