Adverts

Feb 7, 2011

Jod description for new director of tourism

Jod description for new director of tourism: "
Kwako Ndugu Ibrahim Mussa. Kwanza kabisa nakupongeza kuteuliwa kushika wazifa wa Mkurugenzi wa utalii nchini. Ni nafasi kubwa na nina imani kwa uzoefu wako unaweza kusimamia vema rasilimali hii ya Taifa letu. Nikiwa kama mdau katika sekta hii ningependa nikuongezee machache kwenye majukumu yako. 1. Ufanisi wa kazi TANAPA/NCAA na TTB – Washauri watendaji wa idara hizi wapunguze safari za nje na waelekeze taaluma zao kwenye field. Hawa waheshimiwa safari za nje ni nyingi kuliko safari za kwenda field na ndo maana ziwa manyara linakufa, Serengeti bara bara mbovu na ngorongoro wanyama wanazidi kupotea. It is evident kwamba wanyama sasa hivi ni wa kutafuta Ngorongoro/Serengeti saa nyingine hata ni aibu kwa wageni uliowabeba. 2. TTB wawe na information za kutosha kuhusiana na utalii wan chi hii. Mwaka jana nilitembelea ofisi za TTB na foreigner ambaye alikuwa ana dreams za kuwekeza hapa kwetu. Wakati anatoka kwao US kuja TZ ubalozi wetu wa US ulimshauri afike TTB apate information. Ukweli ni kwamba ofisa tulionana nae hakuwa na information za kutosha kuweza kumu impress investor. 3. TANAPA, NCAA, TTB – Wakubwa wajaribu ku delegate kazi ili wanapokuwa nje ya ofisi shughuli ziendelee kama kawaida. Ilinichukua miaka mitatu kupata lease ya plot ndani ya park sababu tu wakubwa wanakuwa hawapo ofisini. Utaambiwa Dar, Swiss, USA, Europe, Neatherlands. 4. Simamia miundo mbinu ya southern corridor – I know the policy is to promote this circuit but how? Kama hakuna miundo mbinu investor gani atakwenda? Waliopo sasa wanalia sababu wame invest ila hakuna returns. (Serenan, Nomad safaris) 5. Uwazi na ukweli kwenye tender – Kuna kampuni mbili tu zimekuwa zikitengeneza barabara ya ngorongoro miaka yote while their performance is poor. Hii barabara ya kuanzia Loduare gate mpaka golini imekuwa ikitengenezwa throughout the year na ni pesa nyingi sana inapotea kwa ajili yaku i maintain. Barabara imekuwa kero kwa tour operators sababu inauwa magari so it affects the margin. 6. Boresha mfumo wa payments cards. The system is very good if it will work successful sababu itapunguza loopholes. Lakini kuna kero kubwa sana kwenye magate kwasababu system mara nyingi huwa inakuwa down na gate clerks wanakuwa siyo flexible moving to plan B which is cash payments. 7. Review fidia za wafugaji/wakulima – Jaribu kuangalia upya fidia za hawa wananchi wanao ishi maeneo ya jirani na parks. Mfano Tarangire kuna bwana shamba lake la watermelon heka mbili lililiwa na tembo lakini baada ya miezi sita akapata fidia tshs 100,000. 8. KARIBU TRADE FAIR – Hebu tujaribu kuipa uzito hii trade fair kwani sasa hivi imekuwa na potentials nyingi sana karibia na Indaba ya south Africa. The whole of east Africa (five regions) wanatupongeza kwa hii fair. Ila tunaomba serikali iipe uzito especially during the fair in may. Imekuwa iki pick from year to year. Ila serikali haioni kama ni kitu cha msingi. Mwaka jana tuliambiwa ingefunguliwa na Mh Rais/PM/VP and all participants were curious to see the guest of honor but finally no one turned out. Trade fair za wenzetu kama ITB, WTM waziri wa wizara husika anafatilia mpaka day to day logistics 9. Okoa ziwa Manyara – fanya environment audit so as to address the problems which are facing this lake as it’s dying a natural death 10. Boards – Mshauri waziri husika hizi boards zetu wawekwe na stake holders ambao wanaweza wakatoa mawazo chanya kama haya. Hayo ni mawazo yangu na nina imani idara hizi zina wataalamu wa kutosha hivi tukiwa wazalendo tutasonga mbele. Asante na kazi njema kaka yangu.
"