Adverts

Feb 9, 2011

Kampuni ya Nokia iko katika wakati mgumu

Kampuni ya Nokia iko katika wakati mgumu: "

Stephen Elop, bosi mpya wa Nokia anayeamini kuwa kampuni hiyo iko kwenye kipindi cha changamoto kuliko wakati mwingine wowote

Stephen Elop, ambaye ni bosi mpya wa kampuni maarufu katika utengenezaji wa simu za kiganjani aina ya Nokia, amesambaza ujumbe wenye kuwaonya wafanyakazi wa kampuni hiyo kote duniani kuwa iko katika wakati mgumu kibiashara pengine kuliko wakati wowote ule kwenye maisha yake.

Bosi huyu ambaye bado angali akitumia fursa zilizopo kufahamiana na wafanyakazi pamoja na wadau wao mbalimbali katika kila kona duniani, ameyasema hayo katika waraka ambao umesambazwa kwenye matawi ya kampuni hiyo takriban duniani kote, ambapo amelinganisha mwenendo wa kampuni yao na wapinzani wao wakuu katika uzalishaji wa simu za viganjani, ikiwemo kampuni ya Apple.

Ametolea mfano wa kuporomoka kwa hisa za kampuni yao katika kipindi cha mwaka 2010 kulinganisha na mwaka 2009, huku washindani wao wakizidi kushika kasi katika kukua kwa thamani za kampuni zao, na kuainisha hilo kama sehemu ya changamoto wanazotakiwa kuzizingatia kama kiashiria cha kuwa kwao kwenye wakati mgumu.

Soma zaidi habari hii pamoja na zingine zenye kuhusiana na hali ya kampuni ya Nokia, kwa kubonyeza hapa

"