Adverts

Feb 23, 2011

LEODGAR TENGA ASHINDA UJUMBE WA CAF!

Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania aka TFF,Leodgar Chillah Tenga ameshinda nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji wa Shirikisho la soka la Africa,CAF kwa tiketi ya Afrika Mashariki na kati kwenye mkutano mkuu wa 33 wa CAF unaofanyika jijini Khartoum-Sudan kwa kupata kura 39 dhidi ya 14 za mpinzani wake Calestin Musabyimana toka Rwanda. Kwa sasa ni Rais wa TFF,Rais wa CECAFA na mjumbe wa Shirikisho la Soka la Afrika-CAF kwa tiketi ya Afrika Mashariki na Kati....Big Up Prezidaaaa!
"