Adverts

Feb 6, 2011

MALAWI WAPIGA MARUFUKU KUPUMUA?

MALAWI WAPIGA MARUFUKU KUJAMBA HADHARANI: "
Kujamba

Malawi kukataza watu kujamba?

Mzozo umezuka nchini Malawi kufuatia mapendekezo kutaka kufikishwa bingeni kuhusu kujamba, kuwa ni kosa.

Waziri wa sheria wa Malawi, George Chaponda amesema muswada huo utakaojadiliwa kuwa sheria ndani ya bunge wiki ijayo, utapiga marufuku kabisa kwa mtu kufanya haja hiyo hadharani. Waziri huyo amekiambia kituo kimoja cha radio nchini humo- kwa maneno yake - 'nenda chooni kama unajisikia kujamba'.

Hata hivyo mkuu wa wanasheria nchini Malawi Anthony Karanga amesema kufanya haja hiyo hakufikii kuharibu hali ya hewa kiasi cha kuwa kosa la jinai.

Mwandishi wa BBC nchini humo anasema wananchi wa Malawi wanajiuliza mapendekeo ya sheria hiyo, iwapo itapitishwa, itatekelezwaje.

"