Adverts

Feb 6, 2011

CHUPUCHUPU KUTUPWA JELA BAADA YA KUBUSU MAKALIO YA MKEWE.

CHUPUCHUPU KUTUPWA JELA BAADA YA KUBUSU MAKALIO YA MKEWE.: " Mwanaume mmoja wa nchini Australia ambaye kutokana na pombe alizokunywa aliamua kumvua kinguvu mkewe nguo zake na kumbusu makalio yake, amenusurika kutupwa jela kwa kufanya shambulizi la kijinsia. Mwanaume huyo ambaye jina lake halikutajwa kutokana na sababu za kisheria mwenye umri wa miaka 48, alikiri kosa lake na kuomba msamaha na hivyo kunusurika kutupwa jela kutokana na kitendo chake cha kuyabusu makalio ya mkewe Mahakama ya mji wa Hobart katika kisiwa cha Tasmania nchini Australia, ilimuona mwanaume huyo ana hatia ya kufanya shambulizi la kijinsia kwa mkewe kwa kumvua nguo kinguvu na kuyabusu makalio yake. Mahakama iliambiwa kuwa mwanaume huyo akiwa amelewa alienda nyumbani kwa mke wake aliyetoroka nyumbani kwake ili waweze kuongea na kumaliza tofauti zao. Mkewe alikuwa amelala kitandani na mara mbili mwanaume huyo alimwambia mkewe alale kifudifudi lakini alipokataa alitumia nguvu kumpindua na kumvua nguo zake za ndani kabla ya kuanza kuyabusu makalio yake huku mkewe akipiga kelele za 'No, No'. Wakati watoto wao walipokimbilia chumbani kuona nini kimemtokea mama yao, mwanaume alitoa maneno ya kashfa. Wakati alipofunguliwa mashtaka ya shambulizi la kijinsia na mkewe na kuhojiwa na polisi, mwanaume huyo alikiri kosa lake na kumuomba msamha mkewe. Mwanaume huyo alijitetea kuwa aliamua kumbusu mkewe makalio kwa kufikiria kuwa kitendo hicho huenda kikaamsha tena cheche za mapenzi yao. Hakimu Olivia McTaggart akitoa hukumu alisema kuwa mwanaume huyo anastahili kutupwa jela lakini aliamua kumhukumu kifungo cha nje cha miaka mitatu kwa masharti ya kutofanya tena shambulizi la kijinsia.
"