Adverts

Feb 2, 2011

Marekani yafuta pambano lake na Misri

Marekani yafuta pambano lake na Misri: "

Maelfu kwa maelfu ya wananchi wameendelea kujazana mitaani wakishinikiza mabadiliko huko nchini Misrikatika miji mbalimbali nchini Misri,

Vurugu zinazoendelea nchini Misri, zimeathiri sekta ya michezo nchini humo baada ya Marekani kuamua kufuta pambano la soka la kirafiki baina ya mataifa haya mawili. Mechi hiyo ilitarajiwa kufanyika jijini Cairo Jumatano ya Februari 09, mwaka huu.

Misri, walikuwa watumie pambano hili kwa ajili ya kujipima uwezo wa kikosi chake ambacho kinatarajiwa kuumana na Bafana Bafara, mwezi machi, kuwania tiketi ya kushiriki michuano ya Mataifa ya Afrika, ya mwaka 2012.

Soma zaidi kuhusu habari hii kama ilivyoandikwa na BBC kwa kubonyeza hapa

"