Adverts

Feb 2, 2011

Mtandao wa matukio ya uhalifu waharibika huko Uingereza

Mtandao wa matukio ya uhalifu waharibika huko Uingereza: "

Mtandao wa Polisi wenye kuonyesha ramani ya matukio mbalimbali ya kihalifu huko nchini Uingereza, umepata hitilafu kutokana na kuzidiwa uwezo. Mtandao huo ambao ulianzishwa mahususi na Polisi nchini humo, kwa lengo la kuainisha idadi na maeneo yenye matukio mengi au machache ya kihalifu katika mitaa mbalimbali ya Uingereza, umelazimika kutokuwa hewani kwa muda baada ya idadi ya watembeleaji kuzidi uwezo wa mitambo inayouendesha.

Taarifa za kipolisi nchini Uingereza, zimeelezea kuwa, tangu ulipotangazwa rasmi, mtandao huo ulivutia takriban watu milioni moja kwa saa sawa na watu wapatao 75,000 kwa dakika.

Soma zaidi habari hii kama ilivyoandikwa na BBC kwa kubonyeza hapa

"