Mjadala wa katiba mpya ambao ulikamilika katika nchi jirani ya Kenya kwa kupiga kura ya maoni (Refferendum) sasa unaelekea kushika moto nchini Tanzania na hivi karibuni kulifanyika kongamano katika chuo kikuu cha Daresalaam nchini Tanzania ambalo lilishirikisha wasomi,wakufunzi na wataalam mbali mbali.
Natumaini ni wakati mzuri wa kuwasikiliza baadhi ya wasomi hawa na wakufunzi wana maoni gani na wewe msomaji uchukue nafasi pia kujisomea katiba hiyo ili uweze kutoa maoni yako na kupata nafasi ya kuwakilishwa katika katiba hiyo na pengine unaweza kujiuliza utaipata wapi usingoje mpaka utumiwe na mtu unaweza kuingia Bongo celebrity.com ndugu yetu Jeff ameweka link ya katiba hiyo nzima unaweza kujisomea pale.
Jenerali Ulimwengu mbunge wa zamani, mwanaharakati na mmiliki wa habari Corporation alikuwa na haya ya kuchangia.
Naye mkurugenzi wa sheria na haki za binadamu wa Chadema na mbunge wa Singida Mashariki kwa tiketi ya Chadema Tundu Lisu pia alikuwa na haya ya kusema.
"