Mbunge Machachari toka Gichugu na waziri wa zamani wa sheria na katiba toka nchini Kenya,Martha Wangari Karua ameingia studio na kuandika verse na baadaye kuingiza Lyrics kwenye Studio iitwayo Click Track Studios pande za Nairobi,kwenye wimbo wa Emanuel Jal ambaye alikua ni askari mtoto aliyepigana toka Sudan ya Kusini uitwao WE WANT PEACE,ambao una ujumbe wa kupiga vita ukabila na Emanuel Jal alimuomba Mh Karua kupitia mtandao wa FaceBook na kukubali....Hope ni mfano mzuri kwa viongozi wengine wa kisiasa hapa kwetu kutoa ushirikiano kama hivi....Ila mwakani 2012,Bi Martha Karua anakusudia kugombea Urais wa Kenya
"