Adverts

Feb 4, 2011

Mmatumbi ni mmatumbi tu: Kolo Toure na Adebayor walipozipiga mazoezini

Mmatumbi ni mmatumbi tu: Kolo Toure na Adebayor walipozipiga mazoezini: "
wachezaji nyota Kolo Toure na Emmanuel Adebayor wa Manchester City wakizipiga baada ya kuchezeana rafu mazoezini. Ugomvi huu inasemekana umeanza toka Desemba mwaka jana wakati Toure akiwa kama nahodha alisikika akiwalaani wachezaji wanaoongea na vyombo vya habari bila mpango. Adebayor, ambaye yuko benchi kwa muda mrefu, inasemekana alikuwa akilalamika kila mara kwamba hali si hali kwake hapo Man City, hivyo akahisi kijembe kimeelekezwa kwake. Kocha wa Manchester City Roberto Mancini na wachezaji wengine wakiamulia zogo hilo. Leo Man City wanakipiga na timu ya zamani ya Toure na Adebayor na redio mbao zinasema Adebayor anataka kuogelea Bwawani.
Kwa chanzo cha habari na picha zaidi BOFYA HAPA
"