Habari zenu binafsi bana...!
Wapendwa, nina swali kwa wataalamu wanijuze...! Nimesikia kwa marafiki zangu kuwa mtoto akiacha kunyonya mapema kunaleta madhara kwa mama na hata inaweza kupelekea kupata kansa ya matiti. Sasa mimi mwanangu ameacha kunyonya miezi 3 iliyopita akiwa na miezi 6. Nimepata wasiwasi kuhusu hayo madhara. Je, ni kweli yaweza kudevelop breast cancer? Na Je, ni kweli kuna sindano natakiwa nichome kukausha maziwa yaliyobaki ili yasileta madhara?
Naombeni majibu tafadhali. Natanguliza shukrani...
"