Adverts

Feb 17, 2011

MWANAMKE AFARIKI DUNIA BAADA YA KUDUNGWA SINDANO ZA KUNENEPESHA MAKALIO!

MWANAMKE AFARIKI DUNIA BAADA YA KUDUNGWA SINDANO ZA KUNENEPESHA MAKALIO!: "
  • Inavyoonekana vuguvugu la kuongeza makalio kwa mabinti haliko kwetu pekee ambako dawa za Kichina ndizo zinasifika kwa kazi hiyo, (japo sina uhakika kama ni kweli). Hapa Marekani mabinti huamua kufanya operesheni kabisa au kudungwa sindano makalioni.
  • Sasa mwanamke mmoja kule Philadelphia amefariki dunia baada ya kupigwa sindano za kunenepesha makalio yake. Inasemekana kwamba yeye na mwenzake walikuwa wamesafiri kutoka London Uingereza kuja kudungwa sindano hizo. Mwenzake alidungwa sindano za kuongeza mahips na yeye hakupata madhara yo yote. Wadungaji wa sindano hizo sasa wanasakwa na polisi.
  • Dada zetu kuweni waangalifu na haya mambo. Na kama kweli kuna hizi dawa za Kichina, mnajua madhara yake (ya muda mrefu) ni nini? Jihadharini.
"