Adverts

Feb 17, 2011

RUSHWA HATIMAYE KUWA SOMO KATIKA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI TANZANIA

RUSHWA HATIMAYE KUWA SOMO KATIKA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI TANZANIA: "
  • Ule mkakati wa kuliingiza somo la rushwa katika mitaala ya shule za msingi na sekondari nchini Tanzania naona umekamilika sasa. Kwa mujibu wa gazeti la Habari Leo la leo, TAKURURU imetia sahihi makubaliano jana kati yake na Taasisi ya Elimu Tanzania tayari kwa kukamilisha uaandaaji wa mitaala hiyo.
  • Ni kweli hatua hii itasaidia kupunguza rushwa? Isije ikawa tunakurupuka tu na halafu tukaishia kuwarundikia watoto wetu masomo bila hata ya kufanya utafiti wa kina kwanza na kuona kama somo hili litakuwa na athari yo yote chanya. Mimi nadhani ili mkakati wo wote wa kupambana na rushwa ufanikiwe, ni lazima ulenge hasa katika kiini cha rushwa yenyewe. Kwa nini kuna rushwa? Ni akina nani wanaotoa na kupokea rushwa; na kwa nini wanafanya hivyo? Vipi kuhusu hizi rushwa 'nono' zinazolitingisha taifa?
  • Bila jitihada zetu kulenga katika kiini chenyewe, sidhani kama kufundishana tu madarasani kutasaidia cho chote. Mbona tumekuwa tukiimba imani na ahadi za mwana TANU (na baadaye CCM) kwamba 'Rushwa ni adui wa haki, sitapokea wala kutoa rushwa' kwa miaka mingi na rushwa ipo tu inashamiri?
    "