Adverts

Feb 9, 2011

Mwandishi wa Guardian ya Uingereza atimuliwa Urusi

Mwandishi wa Guardian ya Uingereza atimuliwa Urusi: "

uke Harding, akiwa katika mitaa ya Moscow, kabla ya kufukuzwa nchini humo

Serikali ya Urusi, imemfukuza nchini humo mwandishi wa habari raia wa Uingereza Bw. Luke Harding, ambaye aliripoti juu ya taarifa za mawasiliano zilizokuwa zimerushwa hewani na mtandao wa WikiLeaks, zilizowakwaza watawala wa Urusi. Habari iliyowakwaza watawala wa Urusi kiasi cha kufikia hatua hiyo ni ile iliyokuwa ikielezea kuwa taifa hilo chini ya raisi wake wa sasa Vladimir Putin, limekuwa kama taifa la kimafia.

Katika ukurasa wake wa Twitter, Harding, ameelezea kuwa serikali ya Urusi imemzuia kuingia Mosccow, ikadhibiti hati yake ya kusafiria, ikamkamata na kumuweka kizuizini kwa muda wa takriban dakika 45 kisha akapakizwa kwenye ndege tayari kurejeshwa kwao Uingereza na kwamba baada ya safari ya kurejeshwa Uingereza kuanza, ndipo alirejeshewa hati yake ya kusafiria.

Soma zaidi kuhusu mkasa uliomkumba kwa kubonyeza HAPA au HAPA.

"