Adverts

Feb 12, 2011

NBC YAJIIMARISHA ZAIDI 2010

mapato ya NB yakua wa asimilia saba mwaka 2010: "
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NBC Bw. Lawrence Mafuru akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu taarifa ya utendaji wa Benki hiyo kwa mwaka 2010. Kulia ni Mkuu wa Huduma za Kibenki Bw. Johan Vermaas.

Mkuu wa Huduma za Kibenki Bw. Johan Vermaas akifafanua jambo kwa waandishi wa habari Kulia ni Kaimu Mkuu wa masoko wa Benki hiyo Bw. Arden Kitomari.

Mapato ya benki ya taifa ya biashara (NBC) kwa mwaka 2010 yameongezeka kwa asilimia saba.

Benki hiyo imepata mapato ya shilingi bilioni 176.5 katika kipindi cha miezi kumi na miwili iliyopita ikilinganishwa na rekodi ya mwaka juzi 2009 ambayo ilikua ni shilingi bilioni 164.2.

Kukua kwa mapato ya kawaida ya NBC ni matokeo ya ukuaji mkubwa wa vitabu vya mahesabu vinavyoonesha ongezeko la 10% kwa mwaka 2010 na kusababisha kupatikana mapato ya jumla ya riba ya Shilingi 123.9 billioni.

Kwa mujibu wa taarifa ya utendaji wa benki, Kitabu cha mahesabu kinaonyesha fedha zote zilizotolewa kama mikopo na zile zilizotolewa kwa ajili ya maendeleo ya sekta binafsi na uwekezaji katika dhamana za serikali, riba za mapato ya mchango ni asilimia 70 % ya mapato, wakati mapato yasiyo na riba ni asilimia 30 % ya mapato ya jumla.

Mapato yasiyo ya riba yalikuwa yanaendeshwa na hazina ya mapato kama vile ada ya huduma na asilimia za faida.

Taarifa hiyo imeendelea kufafanua kuwa licha ya mazingira ya changamoto za kiuchumi kufuatia mtikisiko wa kihistoria wa kimataifa kati ya mwaka 2008/2009, NBC ilikuwa na uwezo wa kuendelea na majukumu yake ya usimamizi fedha na madeni yake yalikuwa na amana ya asilimia 16.53% mwaka huu.

Benki hiyo imesema imedhamiria kuendelea na kuboresha mfumo wa utoaji huduma ili kuwa karibu na wateja na kuwahudumia kwa ufasaha.

Benki ya NBC ina matawi 54 na mashine za ATM ziko kwenye mitandao ya VISA na MasterCard, ili kumwezesha mteja kupata huduma popote.

Benki ya NBC sasa ina mashine za ATM 224 kote nchini na mauzo yamefikia 250 katika kipindi cha miezi 12.

Katika kipindi cha mwaka 2010 NBC imejiingiza katika miradi mikubwa IT kwa lengo la kuboresha teknolojia ambayo imeleta msingi mpya kwa mabenki kwa lengo la kuboresha huduma kwa wateja.

Juhudi zote pamoja na biashara zilipelekea gharama za uendeshaji kuongezeka na kufikia asilimia 35% kwa mwaka, ambapo benki hiyo inaamini kwamba uwekezaji huu ulikuwa muhimu kwa ukuaji endelevu wa benki.

Pamoja na kutokea kuyumba kwa uchumi mwaka 2008/2009, hali hii iliathiri sehemu kubwa ya mikopo hasa ile ya maendeleo na kusababisha matatizo ya mikopo ya ndani kufikia Tsh 34 bilioni.

Hii imetokana hasa na baadhi ya miundombinu ya ukopeshaji kua mibovu.

Katika kipindi cha mwaka uliopita benki hiyo ilijiunga na kundi jipya la mabenki ili kwenda sawa na viwango vya (ABSA), na pia kuhakikisha kwamba inafuata miongozo iliyotolewa na Benki Kuu ya Tanzania.

"