SAKATA la askari kumjeruhi kwa risasi Frida Mgimwa mkazi wa Don bosco Iringa limeanza kuchukua sura mpya baada ya diwani wa kata ya Mkwawa Tobias Kikula na wananchi wa kata ya Mkwawa katika Manispaa ya Iringa kutaka tume iundwe ili kuchunguza sakata hilo kabla ya wao hawajaandamana kwenda kwa mkuu wa mkoa wa Iringa kupinga unyama huo .
Wakizungumza na mtandao huo wa www.francisgodwin.blogspot.com wananchi hao na diwani Kikula wamesema kuwa wamepokea kwa masikitiko makubwa juu ya tukio la mwanamke huyo kutendewa unyama huo na kuomba jeshi la polisi kufanya uchunguzi na kuweka wazi uchunguzi huo kabla ya wananchi kuandamana kwenda kwa mkuu wa mkoa kufikisha malalamiko yao.
Mwanamke huyo kwa sasa anaomba wasamaria wema kumsaidia fedha za matibabu ili kumwezesha kwenda Hospitali kupatiwa matibabu huku akiomba uongozi wa hospitali ya mkoa wa Iringa kuendelea kumsaidia zaidi.