Adverts

Feb 12, 2011

BREAKINGNEWs DIWANI WA NJOMBE MJINI AUGUSTINO MBANGA AMEFARIKI DUNIA

BREAKINGNEWs DIWANI WA NJOMBE MJINI AUGUSTINO MBANGA AMEFARIKI DUNIA: " Marehemu Augustino Mbanga
Chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Njombe kimepata pigo kubwa baada ya diwani wake wa kata ya Njombe mjini Bw Augustino Mbanga kufariki dunia. Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na katibu wa CCM wilaya ya Njombe Bw.Hosea Mbagike zinadai kuwa diwani huyo alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Moyo kwa kitambo kabla ya kulazwa katika hospitali ya wilaya ya Makete Ikonda. Katibu huyo amesema kuwa diwani Mbaga amefariki dunia jana akiwa amelazwa katika hospitali hiyo ya Ikonda na kuwa mazishi yake yanataraji kufanyika leo jumamosi kijijini kake Lupembe . Hata hivyo amesema kuwa kifo cha diwani Mbanga kimeacha pigo kubwa ndani ya familia yake ,chama cha mapinduzi na serikali ya wilaya ya Njombe kutokana na mchango wake kuhitajika zaidi katika kipindi hiki. Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi Amina
"