- Huku kiti cha madaraka alichokalia kikiwa kinawaka moto unaochochewa na maovu ya udikteta wa miaka zaidi ya 40 madarakani, Moammar Gadhafi ama ni mgonjwa au hajaelewa kinachoendelea. Katika hotuba yake ya kipayukaji iliyomalizika muda si mrefu uliopita ametoa matamko ya kushangaza - yakiwemo hayo juu. Huku akiwa mwenye hasira na akigonga meza kwa ngumi, amewaita waandamanaji kuwa ni 'mbwa' na akawaonya kwamba wakae chonjo kwani bado hata hajatoa amri ya risasi ya moto hata moja kufyatuliwa; na akitoa amri hiyo basi Libya nzima itawaka moto. Ameendelea kusema kwamba yeye ni shujaa na kwamba ataipigania Libya mpaka tone lake la mwisho la damu!
- Ametoa mwito kwa wanaomuunga mkono kujitoa mhanga kuanzia kesho na kujitosa mabarabarani ili kupambana na waandamanaji wanaoipinga serikali yake. Ili kujipambanua na wapinga serikali, inabidi wavae 'bangili' za kijani katika mikono yao.
- Amewauliza waandamanaji swali la Kitashtiti kwamba 'nini kimewapata? Mbona tulikuwa tunaishi katika ustawi?' Kwa habari zaidi soma HAPA.
Sikiliza sehemu ya hotuba hiyo hapa chini
"