Adverts

Feb 25, 2011

TAASISI YA ELIMU YA WATU WAZIMA YAZINDUA PROGRAMU YA ELIMU MASAFA.

Balozi wa Sweden nchini Tanzania Bw. Lenant Hjalmaker akizungumza wakati wa uzinduzi wa Programu ya Elimu Masafa uliofanyika leo kwenye jengo la Elimu ya Watu Wazima jijini Dar es salaam, Programu hiyo ya kwanza na ya aina yake hapa nchini itawafanya washiriki wasome huku wakiwa kazini. Katika kundi la Kwanza washiriki 40 kutoka vyuo vya Maendeleo ya Wananchi watashiriki katika kupata Elimu hiyo ambayo wataweza kupata chezti cha Diploma kwa kuanzia, Katika uzinduzi huo kumekuwepo na wageni mbalimbali kutoka Chuo Kikuu Huria, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Wizara ya Wanawake Jinsia na Watoto pamoja na wageni wengine ambao wametoka katika Chuo cha Linkoping University nchini Sweden. Katika picha kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Mama Mahia na kushoto ni Bw. Rajab Majagila Mkurugenzi wa Elimu ya Watu Wazima.
Bwa Johan Arvidsson kutoka Chuo Kikuu Cha Linkoping University cha Sweden akizungumza wakati wa uzinduzi wa progaram hiyo leo.
Wageni waalikwa mbalimbali waliohudhuria katika hafla hiyo.
Wageni kutoka Nchini Sweden ambao walishiriki katika uzinduzi huo.
"