Adverts

Feb 2, 2011

Tanzanian Group kutembelea Mikumi

Tanzanian Group kutembelea Mikumi: "
Kikundi cha vijana marafiki waliounganishwa kupitia mtandao maarufu wa kijamii wa facebook, cha Tanzanian Group, kimeandaa safari ya kitalii kutembelea hifadhi ya Mikumi, february 26 mwaka huu kwa lengo la kuwahamasisha vijana wenzao kujijengea utamaduni wa kutalii kwenye vivutio mbalimbali vilivyoko nchini mwetu.
Taarifa iliyosambazwa na waratibu wa kikundi hicho na Jukwaa Huru kuiona, imeonyesha kuwa gharama za ziara hiyo zitakuwa shilingi za kitanzania alfu hamsini tu kwa kila mtu atakayependa kushiriki katika ziara hiyo huku kukiwa na utaratibu wa kulipia gharama hizo kwa awamu kuanzia sasa hadi siku ya safari itakapowadia.
Taarifa hiyo imeonyesha kuwa gharama hizo zitajumuisha usafiri, malazi, viingilio kwenye hifadhi hiyo pamoja na kumlipa mwongozaji wa msafara wao watakapokuwa wakizunguka huku na kule katika mbuga hiyo kujionea utajiri wa rasilimali ambao taifa letu limejaaliwa.
Taarifa hiyo imeonyesha kuwa watakaokuwa wakihusika katika kukusanya michango kwa ajili ya kufanikisha safari hiyo ni pamoja na Waydael Joseph, anayepatikana kupitia namba 0714808494 pamoja na Amosi Magesa wa 0715274062, lakini vilevile imewakaribisha wadau mbalimbali ambao wangependa kufanikisha safari hiyo kufika kwenye ofisi zao zilizoko Mwenge nyuma ya jengo la Nakiete.
"