Adverts

Feb 12, 2011

Tarehe 11 Februari katika Historia ya Uhuru na Mabadiliko Duniani...

Tarehe 11 Februari katika Historia ya Uhuru na Mabadiliko Duniani...: "
Feb 11, 2011 - Wananchi wa Misri wanamuondoa madarakani Rais wao aliyedumu kwa miaka karibu 30 kwa njia ya mapinduzi baridi - ndani ya siku 18. Feb 11, 2009 - Morgan Tsvangirai wa Zimbabwe aliyeongoza kampeni ya mageuzi Zimbabwe anaapishwa kuwa Waziri Mkuu kufuatia mazungumzo na Robert Mugabe. Feb 11, 1990 - Nelson Mandela aliyekuwa mfungwa kwa miaka 27 chini ya utawala wa Makaburu huko Afrika Kusini anaachiliwa kutoka kifungoni. Feb 11, 1987 - Kufuatia mapinduzi ya yaliyomuondoa Ferdando Marcos huko Phillipines mwaka mmoja kabla na kumuingiza Bi. Corazon Aquino; Katiba Mpya ya Ufilipino inaanza kufanya kazi. Feb 11, 1979 - Kufuatia mapinduzi yaliyomuondoa Shah huko Iran, na umwajigaji wa damu uliofuatia Ayatollah Khomeini anashika madaraka. Feb 11, 1979 - China hatimaye inaruhusu vitabu vya Aristotle, Shakespeare na Charles Dickens! Feb 11, 1975 - Margaret Thatcher anashinda uongozi wa chama cha Conservative huko Uingereza; miaka minne baadaye anakuwa Waziri Mkuu wa kwanza mwanamke wa Uingereza; Akifahamika zaidi kama Iron Lady. Feb 11, 1951 - Kwame Nkrumah anashinda uchaguzi wa kwanza wa Kibunge huko Ghana. Ikumbukwe kuwa wakati anashinda uchaguzi huo Kwame alikuwa kifungoni akitumikia miaka mitatu baada ya kuongoza migomo na maandamano. Feb 12, aliachiliwa ili aunde serikali ya Taifa la kwanza la Afrika chini ya Sahara kuwa huru mwaka 1957. Feb 11, 1929 - Vatican City, taifa dogo zaidi duniani linamegwa kutoka Jiji la Roma huko Italia. Ni tarehe hiyo Musolini alikubali kuiachia Vaticani kuwa ni nchi ya kipapa, na Ukatoliki ukapewa upendeleo maalum huko Italia. Nimekusanya mimi. MY TAKE: Hii tarehe inaonekana imekaa kaa kimabadiliko mabadiliko hivi!
"