TCRA kwa mujibu wa sheria iliyoanzisha mamlaka hiyo ipo kwajili ya kutoa leseni na kuregulate shughuli zote za mawasiliano(simu,radio,internet na televisheni).
Sasa kwa upande wa simu(hususani simu za mkononi/viganjani) kumezuka tabia(ya muda mrefu kidogo) ya makampuni ya simu(Tigo,Vodacom,Zantel na Airtel) kuendesha michezo ya kubahatisha. Ilishakuwepo Timiza Ndoto yako,Shinda Mkoko,Shinda Nyumba na mingine mingi tu!
Tatizo langu na TCRA ni kua haya makampuni yanapata faida kubwa mno kupitia michezo hii at the expense of desperate Tanzanians who want snap life successes. Imagine katika Shinda Mkoko ya Vodacom,kwa wateja milioni 6 wa Vodacom kila mmoja kama alituma meseji(meseji 1 ilikua Tsh 500) ya kujiunga shindano lile,then Vodacom walipata Tsh 3,000,000,000!! Vile vihyundai vilikua 100,na kila kimoja kilikua na thamani ya Tsh 12,000,000,then kwa magari yote Vodacom walitoa Tsh 1,200,000,000 tu na kubakiwa na Tsh 1,800,000,000! Hapo ni scenario ya meseji 1 kwa mara 1 kwa wateja hao milioni 6. So imagine kila mteja alituma meseji zaidi ya 10,kwa scenario iyo Vodacom walitengeneza Tsh. 18,000,000,000! Then kwa muda wa takribani miezi 6 ya shindano lile,hata sitaki kujua ni kiasi gani Vodacom walipata.
Licha ya yote hayo,still TCRA hawachukui hatua yoyote ya kuzuia wizi huo. Sasa Tigo nao wana shindano lao la kushinda gari. Same stupid ploys are being done by Tigo! Still TCRA is quiet!
Haya makampuni yanatumia uroho na tamaa za waTZ kupata mafanikio ya haraka,kutengeneza faida mara trilioni! Hizo zawadi zenyewe washiriki ndo wanazinunua kwa vimeseji vyao. Afu makampuni yanajifanya yanawajali wateja wao kwa kuwapa vizawadi ambavyo wateja wenyewe ndo wamevinunua! Kama wanawajali si watumie faida zao kuwanunulia wateja zawadi!
Kama TCRA hawajaona hilo,basi ndo hivyo nawapa taarifa. Ila kama wanaliona afu wanakaa kimya,then waachie ngazi mara moja,kwani ni wezi na wahujumu uchumi. Wakileta ubishi jamani tuandamane kuwatoa hapo.
SOURCE: JAMII FORUMS
"