Kikosi cha Timu ya Bongofleva kikiwa katika picha ya pamoja jioni hii kwenye uwanja wa Taifa mara baada ya kuinyuka timu ya Bongomovie magoli 2-0 ambayo yalifungwa na mshabuliaji wa timu hiyo mwanamuziki H. Baba , Katika mchezo uliokutanisha waigizaji wa filamu na wanamuziki hapa jijini Dar es salaam ili kuchangia misaada kwa ajili ya watu walioathirika na milipuko ya mabomu iliyotokea hivi karibuni kwenye Kambi ya Jeshi la Wananchi JWTZ ya Gongo la Mboto jijini Dar es salaam.
Mratibu wa Tamasha hilo Ruge Mutahaba akiongea na Crew ya FULLSHANGWE amesema fedha zote zitakazopatikana zitakabidhiwa kwa Kitengo Cha Taifa cha Maafa katika siki itakayopangwa ili kiweze kuwasilisha kwa wahanga hao wa Gongo la Mboto.
Tamasha hilo lilikuwa ni zuri na lilivuta hisia za watu wengi ambao walijitokea kwenye uwanja wa Taifa ili kushuhudia brurdani hiyo huku wakichangia kiasi cha shilingi elfu moja kwa kila aliyeingia kwenye uwanja huo wasanii mbalimbali wenye majina makubwa walijumuika katika tamasha hilo lilikuwa ni zuri na lenye kuvutia nia nina imani litakumbukwa siku zote.
Mshambiliaji Ally Kiba akiondoka na mpira ambao alimpasia mshambuliaji mwenzake H. Baba aliyeandika goli la pili kwa kikosi chake cha Bongofleva.
Mgeni rasmi wa tamasha hilo Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Slaa kushoto akiongozana na Mbunge wa Jimbo la Kinondoni Idd Azzan na Mratibu wa Tamasha Ruge Mutahaba.
Hawa ni waigizaji maarufu sana wakiongozwa na mzee Magali kulia na Chilo wanasadikiwa kuwa walikuwa ndiyo waganga wa timu ya Bongomovie, Eh kumbe uchawi mbele ya soka hausaidii.
Mh jamani kama mnavyoona vimwana walimwagika vyakutosha katika tamasha hilo lakini wote hawa walikuwa wakishabikia Bongomovie kwa kuwa nao ni waigizaji lakini wakaangukia pua.
"