Adverts

Feb 9, 2011

wana ccm marekani wachagua uongozi wa muda

wana ccm marekani wachagua uongozi wa muda: "

Safu ya uongozi wa muda , kutoka kushoto_Misso Temu katibu wa Uchumi na Fedha,Abdallah Nyangasa Katibu mkuu,Novatus Simaba Mwenyekiti na Salum Rajabu Katibu wa Habari,Itikadi na Uenezi

Katika sherehe za kuazimamisha miaka 34 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ,zilizo fanyika Siku tarehe 5, February 2011, Katika jiji la Houston, TX.Uongozi wa muda wa Tawi la CCM-MAREKANI unafuraha ya kuwatangazia wapenzi na wanachama wake wote ufunguzi wa shina Jipya la HOUSTON NO. 1; shina hilo lilichagua viongozi wao wakiwemo ,mwenyekiti Cassius Pambamaji na katibu Shaibu Said.Pia katika sherehe hiyo Tawi lilifanikiwa kuandikisha wanachama wengine wapya kumi na wawili.

Pia ungozi wa Muda wa Tawi unapenda kuchukua nafasi hii kuutangaza uongozi wao ambao utakuwa madarakani kwa siku 120 toka ulipochaguliwa tarehe 2, January 2011.Viongozi hao wa muda ni kama wafuatao;

Novatus Simaba-Mwenyekiti

Abdallah Nyangasa-Katibu

Salum Rajab-Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi

Misso Temu-Kaitbu wa Uchumi na Fedha.

Kazi ya uongozi huu ni kuandaa na kuweka mazingira mazuri ya uchaguzi wa viongozi wa Tawi.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

Salum Rajabu,

Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi, Tawi la CCM-MAREKANI

Abdallah Nyangasa akibadilishana mawazo na Viongozi wa Shina jipya Lambaert na safu nzima ya uongozi
"