Adverts

Feb 23, 2011

wanaume na tabia za ghadafi(rais wa Libya)

WanaJF nimeonelea nianze na hii title ili nieleweke vizuri. Kwa wanomjua rais wa Libya anataka wanaompinga wauwawe ama kufungwa maisha na pia kawaita ni mende(komba mwiko),walevi,wavuta unga,magaidi nk.Kasahau kuwa watu hao hao wlaiokuwa wanamkubali wamemgeuka kwa sera zake mbovu na za kidikteta,anataka yeye ndio awe na sauti ya mwisho kwa kila kitu kinachohusu LIbya bila kujali athari zake. Nasema hivi kwa sababu wanaume wengi tuko hivo katika ndoa zetu.Wakati wa kuchumbia yawezekana ulikuwa na chumba kimoja tu tena cha kupanga na una kitanda kimoja na tv ya nchi 14 tu.Unampata mchumba yy kaamua kukuvumilia kwa jinsi ulivo yy hajali una nn bali anajali upendo wa dhati,kwa kuanza akakuletea jiko na sufuria na kukushauri usile magengeni.Baadae mkaoana na kwa kuwa kila mmoja wenu ana kazi mkaamua kupanga nyumba ya vyumba wiwili huku mkinunua kiwanja na kujenga kibanda chenu cha kuishi na pia kwa watoto mtakaojaliwa.Mungu kawajalia mkapata watoto wa 4 na mnashirikiana kuwasomesha.Sasa we mwanaume baada ya kukaa kwenye ndoa na kujiona sasa we ni kichwa cha nyumba ukaanzisha udikteta ndani ya nyumba,hela za matumizi hutoi kwa vile mke nae ana kazi, mke kaamua kujiongezea elimu huku unamsimanga na haumsaidii ada wala kutunza familia,na pia umeamua kuwa na wa pembeni ambae unampa matumizi yote.Mkeo akiuuliza helaza matumizi unaishia kumtia vibao tena mbele za watoto huku ukimtaka afungashe virago vyake aondoke kwani hana adabu wala heshima na unataka kumleta nyumba yako ndogo kwenye nyumba ulioshirikiana na mkeo kuijenga.Hivi kweli inaingia akilini/ nkisema wanaume tuna akili kama za Ghadafi ntakuwa nimekosea?Hii ni habari ya kweli wanaJF WanaJF nawasilisha.
"