Adverts

Feb 15, 2011

Wasiyoyajua wanaume kuhusu wanawake

Wasiyoyajua wanaume kuhusu wanawake: "

Mnapoamka asubuhi mwambie kuwa alikuwa anakoroma usiku, halafu utashangaa na kugundua fact nyingine kuhusu mwanamke

Kutoka katika blogi moja ambayo imebobea katika kuainisha baadhi ya mambo ambayo ni ya kushangaza kidogo ya World Amazing Informations, nikakutana na mambo kadhaa ambayo kumbe wanaume hawayajui kuhusu wanawake, licha ya kuwa wamezaliwa, kukuzwa na wanaishi nao. Tafsiri iliyotumika yaweza kuwa sio rasmi, lakini imelenga zaidi katika kufanya mambo kueleweka.

1. Wanawake eti siku zote hawana kitu maalum cha kuvaa. Na ndio maana waweza kuta kabati la mwanamke limejaa nnguo na mabegi kadhaa, lakini asubuhi analalamika hana nguo ya kuvaa.

2. Wanawake ni wenye kupenda kulia sana na kila wakati, lakini hawawezi kufanya hivyo kama haupo karibu nao au kama huwezi kusikia kilio chao

3. Wanawake ni viumbe wenye kupenda kuona kuwa duniani kuna watu wabaya zaidi yao, na ndio maana vipindi vingi vya kuelezea mikasa ya kinamama walioonewa vinapata umaarufu sana duniani.

4. Wanawake hupendelea sana kufanya manunuzi, maana hili ni moja kati ya mambo ambayo wanaamini wana udhibiti nayo kuliko jambo lolote duniani

5. Wanawake daima si watu wa kukosea. Huamini kuwa, makosa wameumbiwa wanaume tu, na ndio maana wao hata wakiosa kuomba msamaha ni kwa bahati mbaya japo wakikosewa wasipoombwa msamaha ni tatizo kubwa sana

hapa atakwambia sina viatu kabisa.....wakati kwa mwanaume jozi za idadi hii zinaweza kumchanganya

6. Wanawake wenngi hupenda kuuliza swali la “Je, naonekana vipi hapo?”, japo ukweli ni kwamba hawapendi majibu ya kweli kuhusu swali hili

7. Mwanamke anaweza kujipara hata kama anaenda kufanya kazi ya kunyweshea bustani, kusoma kitabu au kwennda jikoni kupika. Anaweza kukaa mbele ya kioo chake kwa ajili ya kujiandaa kwa haya

8. Mwanamke anaweza kuendesha gari umbali wa maili hata 100, kwa hofu tu ya kupotea kidogo endapo atatumia njia ya mkato yenye uwezo wa kupunguza safari yake kwa maili 50 nzima

9. Wanawake hupenda sana kuongea kwa simu. Anaweza kumtembelea rafiki yake na kuwa naye kwa wiki kadhaa, na anaporejea kwake muda mfupi baadae akampigia rafiki yuleyule na wakaongea masaa zaidi ya matatu kwenye simu.

10. Wanawake hupendelea kuchana nywele zao kabla ya kulala. Jiulize kwanini sasa na utaambiwa wewe hujui kitu.

Haya ni baadhi tu ya mambo ambayo wanaume hawayajui kuhusu wanawake. Mengi zaidi waweza kuyapata kwa kutembelea hapa au pia waweza kupata zaidi kwa kutembelea webu hii.

"