Waziri wa Maji, Profesa Mark Mwandosya (Watatu kushoto) akikata utepe kufungua Tawi jipya la Benki ya CRDB Mwanjelwa Jijini Mbeya. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Benki hiyo Bw.Martin Mmari na Meneja wa tawi hilo Bw. Luila Ephraim. Kulia ni Mkurugenzi mtendaji wa Benki hiyo Dr. Charles Kimei, Mwakilishi wa mkuu wa mkoa wa Mbeya, Kanali Kayombo na Mama Mwandosya.
Waziri wa Maji, Profesa Mark Mwandosya akikabidhi baadhi ya vitanda, magodoro na mashuka kwa mwakilishi wa mkuu wa mkoa wa Mbeya, Kanali Kayombo. Vifaa hivyo vilitolewa na Benki ya CRDB kwa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya wakati wa ufunguzi wa tawi la Mwanjelwa. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Benki hiyo Bw.Martin Mmari na katikati ni Mkurugenzi mtendaji wa Benki hiyo Dr. Charles Kimei.
Waziri wa Maji, Profesa Mark Mwandosya, mwakilishi wa mkuu wa mkoa wa Mbeya Kanali Kayombo, Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB Bw.Martin Mmari, Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya CRDB Dr. Charles Kimei na Mama Mwandosya wakiwa pamoja na wafanyakazi wa Benki hiyo tawi la Mwanjelwa muda mfupi baada ya ufunguzi wa tawi hilo.