Adverts

Mar 3, 2011

ANGALIZO LA DK. AUGUSTINO L. MREMA KWA CHADEMA NA UHAMASISHAJI WA MAANDAMANO.

Mbunge wa Jimbo la Vinjo, Mwenyekiti wa Chama cha TLP na mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Fedha za Serikali za Mitaa Dk. Augustino Lyatonga Mrema akizungumza na waandishi wa habari leo kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo wakati alipotoa angalizo kwa chama cha CHADEMA kutokana na mikutano yake inayohamasisha maandamano akisema kuhamasisha maandamano kunaweza kuleta uvunjifu wa amani kama ilivyotokea kwa nchi za Madagascar, Misri, Tunisia na sasa Libya.
Dk. Mrema ameongeza kwamba kwa mkawaida mkiiangusha serikali bila kufuata utaratibu wa kikatiba upo uwezekano mkubwa wa kuleta vurugu katika nchi kama ilivyotokea kwa nchi hizo za kiafrika ambazo hata walipoondolewa watawala ambao walikuwa hawatakiwa bado hakuna utulivua na mahali pengine jeshi limepata mianya ya kuchukua madaraka kwa lengo la kuhakikisha usalama wa nchi zao kama ilivyotokea kwa Misri ambayo kwa sasa inaongozwa na Jeshi, katika picha kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho Mh. Hamad Tao.
"