Nimejiunga na TANU tangu mwaka 1966, mimi ni mwana CCM tangu
kuanzishwa kwake 1977 na ni mjumbe wa NEC
Sina uhusiano mbaya na UVCCM, sina uhusiano mbaya na yeyote ambaye ni
mwana CCM.
Napenda kuongelea kuhusu 2015, sijaamua kama nitagombea au sitagombea
Wananchi ndio wenye uwezo wa kila jambo katika nchi, wananchi ndio
wanaopiga kura na ndio wanaoamua nani awe kiongozi na nani asiwe.
Makundi matatu yanayoamua nani awe kiongozi ni WANANCHI, CHAMA
anachotoka mwanasiasa na DOLA
Kwanini nimewaita?
Kumeibuka malumbano ndani ya CCM na UVCCM kutokana na matamshi ambayo
yanakanganya na mimi ni mmojawapo ambaye nimeshambuliwa sana.
Nipo hapa kwa niaba yangu mwenyewe, sijatumwa na yeyote na SIMSEMEI
YEYOTE. Nipo hapa kama Frederick Sumaye.
Ningeyapeleka kwenye chama hasa NEC lakini kwakuwa na wenzangu
wameanza kwa mtindo wa kuitisha vyombo vya habari nami nafuata
utaratibu huo
Lengo si kushindana wala kupimana nguvu, lengo ni kuweka uwazi kwa
wananchi watambue uhalisia
Baada ya kuona wananchi wanavyoyapokea maandamano ya CHADEMA na kwa
hamasa kubwa nilishauri CCM itoe ushirikiano kwa serikali kwa kuyajibu
wanayotoa CHADEMA ili kuweza kuweka hali halisi. Mimi kusema CCM
ifanye sikumaanisha MIMI SIMO.
Aidha, sijasema serikali isifanye kazi yake. Waziri Wassira amefanya
kazi ya serikali vema tu
Katika utaratibu wa kawaida, chama kinafanya kazi yake baadae serikali
inakuja kumalizia yanayobakia. Kama kazi ya siasa haijafanyika vema na
chama basi serikali hubeba lawama zisizostahili.
Malumbano ya kisiasa hujibiwa kisiasa, CCM walitakiwa kuwajibu CHADEMA
na si kazi ya serikali kufanya kazi ya kisiasa
CCM inafahamu kazi ya kisiasa na kimekuwa kikifanya hivyo tangu
zamani. Viongozi wetu wamekuwa wakifanya hivyo kwenye kila ngazi. Ni
shughuli ya chama na haihitaji maamuzi ya vikao.
Akiongea Sumaye linaonekana tatizo kubwa na tena ni utovu wa nidhamu.
Nimeshutumiwa na hata kutukanwa na wengine ndani ya chama
Nifafanue:
Nimeshutumiwa kuwa namshutumu mwenyekiti wa chama. Nilijibu nikadhani
mambo yameisha kumbe ndo kwanza yameanza.
Nimeshutumiwa na UVCCM Pwani kuwa - Sumaye na Lowassa wana mpango wa
kukivuruga chama ili wafikie malengo yao 2015
Kama Lowassa na Sumaye wanautaka urais 2015, kwanini washirikiane?
2015 kutakuwa na marais wawili?
Hakuna sehemu hata moja ambapo niliwahi kumtaja rais katika maongezi
yangu, madai kuwa namtukana na kumchafua rais ni tuhumu za uwongo
kabisa
UVCCM wanadai sisi tumeshiba na sasa tumevimbiwa... Tuwaache nao wale
kama sisi.
Haya ni matusi na kejeli na inasikitisha sana
Ina maana UVCCM wana mgombea wao ndo maana wengine tunaonekana kero
kwao kwani tunamvurugia mtu wao. Vijana wenye tamaa ya KULA ni hatari
kwa taifa
Eti vijana wanataka wamweke mtu wao ili wale? Imenishtua sana!
Wanadai tunakibomoa chama, wanadai kuwa tunataka rais atoke kaskazini.
Kwa madai yao nchi itaendelea kusonga mbele na wanatupa pole
tunaodhani rais lazima atoke kaskazini.
Ubaguzi huu wa ukanda tena kutoka UVCCM mkoa wa Pwani usipochukuliwa
hatua utalipeleka pabaya taifa!
UVCCM wana mpango wa kupambana kina Sitta na Sumaye. Wanataka hawa
wasipewe nafasi katika chama, wanadai watapigana ndani na nje ya chama
kuhakikisha watu hawa hawapewi nafasi.
My comment:
Sitta yashaanza kumkuta ya UVCCM huko Tabora!
Kuna maoni mengine yanaweza kuwa na athari kwa chama hivyo ni juu ya
kiongozi husika kuangalia athari ya kutoa maoni husika.
Serikali yoyote iliyochaguliwa kidemokrasia LAZIMA itasemwa na
kukebehiwa. Kiongozi yeyote na chama chochote kilichochaguliwa
kidemokrasia, kitasemwa na watu watakikebehi. Si ajabu
Nimeshtushwa SANA na kauli ya UVCCM mkoa wa Pwani kuwa suala la rais
ajaye 2015 lipo mikononi mwa rais Kikwete! Hili linanishtua, siamini
kama rais Kikwete anamjua rais ajaye 2015
Sasa hivi mtu yeyote akiongea ndani ya CCM ataambiwa anautaka urais,
hii inaweza kuwaziba wengi midomo
Nawaomba watanzania, yeyote atakayejaribu kutumia njia za udanganyifu
kwa RUSHWA, KUTENGANISHA WATU, tumkatae kwa nguvu zote
Tunakosa muda wa kujielekeza katika mambo ya msingi tunaanza siasa za
kupakana matope - Sumaye
Nategemea nimeeleweka, sitarajii kuibua malumbano na sitarajii kurejea
kuongea na waandishi juu ya hili. Mimi ni mwana CCM na sipo chama
chochote cha siasa zaidi ya hiki.
Mungu Ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika
MASWALI
SWALI: Kwanini hujaandika barua CCM?
JIBU: Mimi sijaandikiwa barua, sijibu kwa barua
SWALI: Mtu akikutukana ujue KATUMWA NA BABA na ndo maana baba kakaa
kimya. Kwanini usijiondoe CCM?
JIBU: Ukiona mtoto anamtukana mtu mzima uelewe ametumwa ama
anamtukanisha mtu mzima lakini kwa hili la sasa yote yamo. Maana
hatujakaa kutuma vijana. Siwezi kutoka CCM sababu ya vijana
SWALI: Toka miaka ya 70 kwanini watu wa kaskazini wanasemwa vibaya?
Hawafai? Toa ufafanuzi kuhusu kauli yako ya 2005 kuwa ATAKAYEINGIA KWA
KUCHAFUA WATU KWA KALAMU ATATUMIA VISASI kuongoza.
JIBU: Nilishasema awali, ubaguzi wa kimaoeneo ni hatari sana na si kwa
kaskazini tu. Kuhusu suala la U-Kaskazini haina maana maana haijawahi
kutoa rais hata akitokea Bagamoyo leo akawa anafaa hakuna neno.
Tusitazame watu kwa wanakotokea ama dini zao na rangi zao. Hata
bungeni kuna kauli za kibaguzi, tumezikemea bila kujali eneo.
Pili, ya 2005: Ni tabia mbaya kuchafuana hata kama ni udiwani,
niliyasema na bahati hayajatokea.
SWALI LA KUBENEA: Vijana wamejitokeza kutetea mafisadi, unatoa rai
gani? Lakini ultimatum wanazotoa si sahihi, labda watoe ushauri.
JIBU: Vijana wanatetea mafisadi ama nani, sijui... ila misemo yao
inanitisha
SWALI LA BBC: Imejitokeza kuzungumza mambo ya chama nje ya chama, kama
chama mnalionaje hili haliwaaibishi?
JIBU: Future ya CCM ni nzuri ila kuna mambo LAZIMA yafanyike. Yale
madhaifu lazima tuyaondoe.
kutoka www.mjengwa.blogspot.com
|