Adverts

Mar 2, 2011

HIZI LUGHA SIKU ZITATUTOKEA PUANI? HIVI TUNAMFURAHISHA NANI?

Sifurahishwi wala sipendezwi la mabango yanayokula kodi ya wananchi wa Tanzania halafu yanalenga kumfurahisha mzungu badala ya ujumbe huu kumlenga mwananachi wa kawaida anayefika kupata huduma kwenye hospitali hii ili apime na kulinganisha na dhamira na maono yake kama inavyotafsiriwa kwenye bango lililoandikwa kwa kimombo wakati hospitali inalaza wasafwa, wanyakyusa, wandali, wakinga na wamalila kutoka wilaya za Mkoa wa Mbeya ambako hakuna hata kabila hata moja ambalo linatumia kingereza kama lugha yake labda kiswahili ambacho huwaunganisha wote.