Kamishna wa polisi nchini Kenya Mathew Iteere amewaonya wamiliki wa maduka makubwa na hoteli kuwa macho kufuatia vitisho vilivyotolewa na kundi la al Shabaab la Somalia, ambalo tayari limewahi kufanya shambulio moja la kimataifa.
Hata hivyo Kamishna Iteere amesema polisi imeimarisha usalama katika maeneo ya umma baada ya kutolewa kwa kitisho hicho.
Msemaji wa kundi la al Shabaab Sheikh Ali Mohammed Rage amesema Kenya italipa kwa kuwasaidia wanajeshi wa serikali ya mpito ya Somalia na washirika wake kuzishambulia kambi za wapiganaji nchini Somalia.
Kundi la al Shabaab limedai kuhusika na mashambulio mawili ya mabomu katika mji mkuu wa Uganda – Kampala, wakati mashabiki walipokuwa wakitazama mechi ya fainali ya soka ya kombe la dunia mnamo Julai 11 mwaka jana ambapo watu 76 waliuawa.
"