Watoto watatu pamoja na wazazi wao wote wakiwa raia wa Denmark wametekwa nyara na maharamia ambao wameteka boti waliyokuwa wakisafiria katika bahari ya hindi.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Denmark amesema watoto hao wanaumri wa kati ya miaka 12 na 16, na kuwa baada ya kutekwa boti hiyo imeonekana ikielekea Somalia.
Utekaji nyara imekuwa ni biashara yenye faida kubwa nchini Somalia, ambapo makundi ya maharamia yamekuwa yakidai mamilioni ya dola kama malipo ili kuwaachia mateka.
Wiki iliyopita kikosi cha askari wa majini cha kukabiliana na uharamia cha Umoja wa Ulaya kilisema maharamia wanashikilia jumla ya meli 31 na mateka 688.
"