Adverts

Mar 4, 2011

libeneke jipya la mbeya yetu

Salam mjomba Ankal,
Natumai ya kua utakua mzima wa njema afya mimi pia niko salama kabisa, kwanza hongera sana kwa kazi zako za blog ikiwa ni pamoja na kutuletea habari mbali mbali za nchini kwetu, Duniani burudani na michezo big na Mwenyezi Mungu akubariki uendelee mbele zaidi wewe pamoja na timu yako nzima ya matukio.
Kwa niaba ya timu nzima ya Mbeya yetu blog,tulikua tunaomba msaada wako wa kututambulishia libeneke letu jipya la Mbeya yetu, Tunatanguliza shukrani zetu. Asante sana.
JINA LA BLOG: MBEYA YETU
Tunapenda kulitambulisha wadau wote libeneke jipya la Mbeya Yetu ambapo nia na malengo ni kuwaletea habari mbali mbali kutoka Jijini Mbeya, Tanzania na Duniani kwa Ujumla ikiwa unatukio la aina lolote usisite kututumia kupitia mbeyayetu@yahoo.com . karibuni nyote na asanteni kwa kututembelea.
Kwa pamoja tunaweza.
"